Vita Ukanda wa Gaza vimesababisha ulemavu kwa watoto 21,000
3 Septemba 2025Hayo ni kwa mujibu wa Kamati ya haki za watu wenye ulemavu ya Umoja wa Mataifa. Kamati hiyo imesema watoto wasiopungua 40,500 wamepata majeraha yanayotokana na vita na nusu ya hao wamepata ulemavu. Kamati hiyo imesema pia kuwa amri za Israel za kuwataka watu waondoke makwao wakati wa vita mara kadhaa zimeshindwa kuwafikia watu wenye ulemavu wa kuona na wa kusikia
Ripoti hiyo imetolewa wakati Wapalestina 24 wameuawa usiku wa kuamkia Jumatano kutokana na mashambulizi ya Israel. Hospitali ya Nasser imthibitisha kuwa imepokea miili 10 ukiwemo mmoja wa mtoto. miili mingine 14 imepokelewa katika hospitali ya Shifa katika Ukanda wa Gaza.
Katika hatua nyingine yamefanyika maandamano makubwa nchini Israel kulaani hatua ya kuitwa kwa maelfu ya wanajeshi wa Israel ili washiriki katika operesheni ya kuutwaa mji wa Gaza. Waandamanaji wanahofia hatua hiyo itahatarisha maisha ya mateka wanaoendelea kushikiliwa kwenye Ukanda wa Gaza.