UchumiAngola
Umoja wa Mataifa wataka uchunguzi baada ya maandamano Angola
1 Agosti 2025Matangazo
Ghasia hizo zilizuka siku ya Jumatatu, kupinga ongezeko la Julai 1 la gharama ya mafuta katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta na ambalo mamilioni ya watu wanaishi katika umaskini.
Msemaji wa Ofisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Thameen Al-Kheetan kwenye taarifa yake ameitaka mamlaka nchini Angola kufanya uchunguzi wa haraka, wa kina na huru kuhusu vifo hivyo pamoja na ukiukaji wa haki za binadamu, wakati wa maandamano hayo.
Kulingana na ripoti rasmi, zaidi ya watu 1,000 wamezuiliwa.
Haya yanatajwa kuwa ni machafuko mabaya kuwahi kutokea katika miaka kadhaa kwenye taifa hilo la kusini mwa Afrika.