SiasaAsia
UN:Taliban ikomeshe ukandamizaji dhidi ya wanawake
8 Julai 2025Matangazo
Tamko lililotokana na azimio hilo limeelezea wasiwasi mkubwa kuhusu hali mbaya na kusambaa kwa ukandamizaji wa wanawake na wasichana wote nchini humo. Limeutaka utawala wa Taliban ulioingia madarakani mwaka 2021, kuacha kuwabagua wanawake na watoto katika masuala ya elimu, ajira na maisha ya umma.
Nchi 116 zilipiga kura kuunga mkono azimio hilo wakati Israel na Marekani zimelipinga. Nchi nyingine 12 zikiwemo Urusi na China hazikupiga kura. Chini ya Taliban, wanawake wa Afghanistan hawaruhusiwi kupata elimu kuanzia darasa la saba na kuendelea
Mwezi Desemba mwaka uliopita, utawala huo uliwapiga pia marufuku wanawake kupata mafunzo kwenye sekta ya afya japokuwa baadhi ya shule zinatoa mafunzo hayo kinyume na maagizo.