SiasaSudan
Umoja wa Mataifa watahadharisha juu ya maafa huko Sudan
20 Juni 2025Matangazo
Katika taarifa yake aliyoitowa Ijumaa, Turk ametanabahisha juu ya kutokea athari kubwa kutokana na uhasama unaoendelea katika majimbo ya Darfur Kaskazini na Kordofan. Amesema hali hiyo inazidi kuwa mbaya kutokana na kutowajibishwa kwa wahusika.
Na katika nchi jirani ya Sudan Kusini, Umoja wa Mataifa umesema upungufu wa fedha umelilazimisha shirika la uhamiaji kuahirisha maunganisho muhimu ya usafiri katika nchi hiyo na kuwaacha watu wanaokimbia vita wakiwa wamekwama. Sudan Kusini imetumbukia katika vita na umasikini tangu ipate uhuru mnamo mwaka 2011.