MigogoroKenya
UN yasikitishwa na mauaji ya waandamanaji nchini Kenya
8 Julai 2025Matangazo
Msemaji wa Ofisi ya Haki ya Umoja wa Mataifa Ravina Shamdasani ameelezea hofu ya umoja huo mbele ya waandishi wa habari mjini Geneva.
"Tumesikitishwa sana na mauaji ya jana ya takriban watu 10 pamoja na uporaji na uharibifu wa mali nchini Kenya . Polisi na vikosi vingine vya usalama vilikabiliana na maandamano hayo yaliyogubikwa na vurugu katika mji mkuu Nairobi na takriban kaunti nyingine 16. Risasi za moto, mabomu ya machozi na maji ya kuwasha vilitumika."
Shamdasani amesema Mkuu wa Ofisi ya Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ametoa wito wa kudumisha uvumilivu, utulivu na kuheshimiwa kwa uhuru wa kujieleza na mikusanyiko ya amani nchini Kenya.