MigogoroAfrika
UN yashtushwa na kiwango cha mauaji ya raia Sudan
1 Februari 2025Matangazo
Katika taarifa yake ya Ijumaa, Turk amesema kuwauwa raia wasio na hatia au mtu yeyote asiyehusika moja kwa moja katika mvutano ni uhalifu wa kivita, na ni kinyume cha sheria ya kiutu ya kimataifa.
Soma zaidi: UN yaonya uwezekano wa janga la kibinadamu al Fashir
Kauli ya Turk imeUN yaonya uwezekano wa janga la kibinadamu al Fashirtolewa wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likilaani vikali mashambulizi yanayoshika kasi mjini El-Fasher na kutaka vita visitishwe kati ya pande hasimu. Vita kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF vilivyoanza Aprili 2023 vimewaua maelfu ya watu na vimesababisha wengine milioni 12 wayakimbie makazi yao.