MigogoroMashariki ya Kati
Wafanyakazi 19 wa UN wanashikiliwa na waasi wa Kihouthi
3 Septemba 2025Matangazo
Kulingana na msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephen Dujarric wafanyakazi 18 kati ya hao ni wa Yemen na mmoja ni wa Kimataifa. Dujarric amewasilisha wito wa Umoja wa Mataifa unawotaka waasi wa Kihouthi kuwaachilia wote inaowashikilia bila masharti. Waasi wa Kihouthi walizivamia ofisi za mashirika ya Afya, Chakula na Watoto ya Umoja wa Mataifa mjini Sanaa na kuwateka wafanyakazi baada ya Israel kumuuwa Waziri Mkuu wao Ahmed al-Rahawi na mawaziri kadhaa katika shambulio Alhamisi iliyopita.