Umoja wa Mataifa wapinga utanuzi wa vita Gaza
8 Agosti 2025Matangazo
Msemaji wa umoja huo Farhan Haq amesema mjini New York kwamba wanasimama kidete dhidi ya hatua zozote za kuongeza machafuko huku mzozo huo ukiwa umesababisha vifo vya watu zaidi ya 60,000 katika kipindi cha karibu miaka miwili ya mapigano.
Haq pia alisema mateso ya kibinadamu yamefikia viwango vya juu vya kutisha na kuna uwezekano watu zaidi wakafa kutokana na njaa kama mzozo huu utaendelea kuwa mbaya.
Kauli hizi zinakuja baada ya baraza la usalama la Israel kuridhia mpango wa waziri mkuu Benjamin Netanyahu wa kuukalia Ukanda wa Gaza na kulipokonya silaha kundi la wanamgambo wa kipalestina la Hamas.