Umoja wa Mataifa walaani mashambulizi ya jeshi la Myanmar
11 Aprili 2025Matangazo
Afisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya haki imelaani mashambulizi yanayofanywa na jeshi la Myanmar licha ya kuwepo makubaliano ya usitishaji mapigano yaliyotangazwa kufuatia tetemeko kubwa la ardhi la mwezi uliopita, lililowaua watu zaidi ya 3,600.
Msemaji wa afisi hiyo Ravina Shamdasani amesema katika taarifa mjini Geneva kwamba katika wakati ambao nguvu zinatakiwa kuelekezwa katika kuhakikisha msaada wa kibinadamu unafika katika maeneo ya janga, jeshi badala yake linafanya mashambulizi.
Shamdasani amesema kamishna mkuu anayeshughulikia masuala ya haki za binadamu wa umioja huo Volker Turk analitaka jeshi liondoshe vizuizi vyovyote katika upelekaji na usambazaji wa msaada wa kibinadamu na likomeshe operesheni zake za kijeshi.