MigogoroAfrika
UN: Kuna ongezeko la wakimbizi wa Sudan wanaoingia Chad
7 Mei 2025Matangazo
Shirika hilo limesema takriban watu 20,000 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wamekimbilia Chad katika wiki mbili zilizopita kutokana na kuongezeka kwa ghasia katika jimbo la Darfur hasa kwenye mji wa El-Fasher, na kusisitiza kuwa kuongezeka kwa idadi hiyo kumezua hali ya kutisha mpakani.
Soma pia: Umoja wa Mataifa waonya kuongezeka kwa wakimbizi wa Sudan
Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa katika muda wa wiki tatu zilizopita, zaidi ya raia 540 wamethibitishwa kuuawa huko Darfur Kaskazini, huku vita kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF vikiendelea kusababisha maafa makubwa na sasa vikiwa vimepamba moto katika mji wa Port-Sudan.