Umoja wa Mataifa waanza kupambana na taka za plastiki
5 Agosti 2025Valdivieso, mwanadiplomasia wa Ecuador ameitoa kauli hiyo Jumanne mbele ya wawakilishi kutoka nchi 180 waliokusanyika Geneva, Uswisi, katika juhudi za kujaribu kufikia mkataba wa kihistoria wa kutokomeza taka za plastiki, ambazo ni kitisho kwa maisha.
Amesema wanakabiliana na mzozo wa kimataifa na kwamba uchafuzi wa plastiki unaharibu mifumo ya ikolojia, unachafua bahari na mito, unatishia viumbe hai, unadhuru afya ya binaadamu, na pia unawaathiri walio hatarini zaidi.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, Inger Andersen amesema mazungumzo kati ya kanda tofauti na makundi yenye maslahi yameibua msukumo. Kwa mujibu wa Andersen, nchi nyingi ambazo amezungumza nazo, zilisema zinakwenda Geneva kufikia makubaliano.
Inatarajiwa kuwa mkataba huo unaweza kusainiwa mwaka ujao, 2026.