UN: Iran imetekeleza adhabu ya kifo kwa watu 841 mwaka 2025
29 Agosti 2025Matangazo
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Ravina Shamdasani amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa hali halisi huenda ni mbaya zaidi kutokana na serikali ya Tehran kukosa uwazi. Ameionya Iran kuacha kutumia hukumu ya kifo kama chombo cha vitisho inayozilenga jamii za walio wachache na wahamiaji. Amesema kwa sasa watu 11 wanakabiliwa na hukumu ya kifo nchini humo wakiwemo sita walioshitakiwa kwa uasi. Msemaji huyo wa Umoja wa Mataifa amelalamikia hasa kuhusu kuwaua watu hadharani akisema ofisi yake ina kumbukumbu ya mikasa saba ya aina hiyo.