Umoja wa Mataifa umelaani mauaji ya raia Sudan
4 Aprili 2025Matangazo
Kikundi cha Emergency Lawyers, siku ya Jumatatu kiliripoti kuwa jeshi la Sudan limefanya mauaji dhidi ya raia mjini Khartoum na Jebell Aulia, kwa madai kuwa wanahusishwa na kundi la waasi la RSF.
Soma pia:Mkuu wa haki wa UN ashtushwa na mauaji ya kiholela Sudan
Video iliyochapishwa na shirika hilo ilinasa matukio mengi ya watu, wengine wakiwa wamezibwa macho, wakiuawa kwa kupigwa risasi na wanaume waliovalia sare za kijeshi na wengine wakiwa wamevalia kiraia.
Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu, Volker Türk amesema amesikitishwa sana na habari hizo na akalitaka jeshi la Sudan kusitisha mauaji ya kiholela.