JamiiUmoja wa Falme za Kiarabu
Umoja wa Falme za Kiarabu warikodi viwango vya juu vya joto
23 Mei 2025Matangazo
Umoja wa Falme za Kiarabu umeorodhesha Ijumaa (23.05.2023) viwango vya juu vya joto hadi nyuzi joto 50.4. Ikiwa ni viwango vya juu kabisa kwa mwezi wa Mei katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili tangu taifa hilo lianze kuorodhesha rasmi vipimo vya hali ya hewa mnamo mwaka 2013.
Kulingana na Kituo cha Kitaifa cha Hali ya Hewa, NCM, viwango hivyo vimezidi vile vya nyuzi joto 50.2 vilivyoorodheshwa mwezi Mei mwaka 2009.
Umoja wa Falme za Kiarabu umekuwa ukikabiliwa na hali ya joto kali kuliko kawaida wakati wa msimu wa kiangazi.