Umoja wa Afrika wasifu mkataba kati ya Rwanda na DRC
29 Juni 2025Matangazo
Umoja wa Afrika umesema hiyo ni "hatua muhimu" katika kuleta amani eneo la mashariki mwa Kongo lililokumbwa na machafuko kwa zaidi ya miongo mitatu.
Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf, ambaye alishuhudia kutiwa saini kwa makubaliano hayo mjini Washington siku ya Ijumaa, amepongeza hatua hiyo muhimu pamoja na juhudi zote zinazolenga kudumisha amani, utulivu na maridhiano katika eneo hilo.
Aidha, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amepongeza pia hatua hiyo pamoja na jukumu la Marekani katika kusimamia suala zima la upatanishi. Mkataba huo hauelezei kwa uwazi mafanikio ya kundi la M23 katika eneo lililoharibiwa na miongo kadhaa ya vita lakini unaitaka Rwanda kukomesha "hatua zake za kujihami".