SiasaSudan
AU yaonya kuhusu hatari kubwa ya kugawanyika Sudan
12 Machi 2025Matangazo
Umoja wa Afrika umelaani hatua hiyo ya Wanamgambo wa Rapid Support Forces - RSF na washirika wake wa kisiasa na kijamii ukisema inaweka hatari kubwa ya kugawanyika kwa nchi ya Sudan.
Umoja wa Afrika umeyataka mataifa yote wanachama, pamoja na jumuiya ya kimataifa, kutoitambua serikali yoyote au chombo chochote kinzani kinacholenga kuigawanya na kuitawala sehemu ya mipaka ya Jamhuri ya Sudan au taasisi zake.
Umoja wa Ulaya pia ulisisitiza dhamira yake kwa umoja na mamlaka ya Sudan. Hivi karibuni, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilizungumzia wasiwasi wake kuhusu mpango huo wa RSF na washirika wake.
Lilitahadharisha kwamba hatua hiyo huenda ikazidisha vita na mgogoro wa hali ya kibinadamu nchini Sudan.