Umoja wa Afrika waonya dhidi ya kugawika kwa taifa la Kongo
16 Februari 2025Waasi hao tayari wanaudhibiti mji wa Goma waliouteka mwishoni mwa mwezi Januari.
Kamishna wa amani na Usalama wa Umoja wa Afrika Bankole Ade-oye, amewaambia waandishi habari kwambaumoja huo hautaki kuona taifa hilo likigawika. Bila ya kuitaja Rwanda moja kwa moja, Adeonye alitoa wito wa kuondolewa mara moja waasi wa M23 pamoja na wanaowaunga mkono katika miji yote ya Kongo ikiwemo uwanja wa ndege wa Goma.
Guterres ahimiza maeneo ya Kongo kuheshimiwa na vita vya kikanda kuzuwiwa
Mapigano yanayoendelea Kongo yameyatia wasiwasi mataifa jirani na yale ya Magharibi kuhusu kutanuka kwa mzozo huo. Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika unaofanyika mjini Addis Ababa Ethiopia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema ni lazima vita hivyo vizuwiwe kuingia kuwa mzozo wa kikanda.