Umoja wa Afrika waondoa vikwazo dhidi ya Gabon
1 Mei 2025Umoja wa Afrika umesema umeondoa vikwazo dhidi ya Gabon baada ya taifa hilo la Afrika ya kati kusimamishwa uanachama wa umoja huo kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 2023.
Kiongozi wa mapinduzi hayo Brice Oligui Nguema aliahidi kuirejesha nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta kwenye utawala wa kiraia baada ya kipindi cha mpito cha miaka miwili na mapema mwezi huu alichaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo kwa zaidi ya asilimia 94 ya kura.
Soma zaidi:Wafadhili waahidi euro milioni 800 kwa ajili ya Sudan
Taarifa ya AU imesema Gabon sasa inakaribishwa "kurejesha mara moja ushiriki wake katika shughuli" za umoja huo huku Rais wa Gabon Brice Oligui Nguema akiandika katika mtandao wa Facebook kwamba anahisi "fahari kubwa" kwamba nchi yake imerejeshwa tena AU.
Mbali na hilo, Brice Oligui Nguema anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa Gabon siku ya Jumamosi ya Mei tatu.