JangaKimataifa
UM: Ukatili wa watoto kwenye mizozo ulizidi 2024
20 Juni 2025Matangazo
Ripoti hiyo iliyochapishwa jana inasema mwaka 2024 visa vya ukatili watoto kwenye maeneo hayo vilipanda kwa asilimia 25 ikilinganishwa na mwaka 2023.
Kulingana na ripoti hiyo, kulikuwa na matukio 41,370 ya ukatili wa watoto yaliyorikodiwa mwaka uliopita kiwango ambacho ndio kikubwa zaidi tangu kuanza kuandaliwa ripoti hiyo karibu miaka 30 iliyopita.
Mzozo wa Ukanda wa Gaza umetajwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya visa vya ukatili na madhila kwa watoto. Umo pia mzozo wa Kongo, vita nchini Ukraine, Sudan, hali ya machafuko ya Haiti na usajili watoto kwa nguvu kwenye biashara haramu ya dawa za kulevya nchini Colombia.