UM. Uchaguzi Afghanistan Septemba
27 Machi 2004Matangazo
NEW YORK: Serikali ya Afghanistan na Umoja wa Mataifa zimekubaliana kuuakhirisha hadi mwezi wa Septemba ule uchaguzi wa Rais na bunge uliokuwa ufanyike Juni, waliarifu maafisa wa UM. Huenda Rais wa mpito Hamid Karsai ataitangaza tarehe rasmi ya uchaguzi huo utakapohudhuria Mkutano wa Afghanistan mjini Berlin katikati ya wiki ijayo. Itakuwa vigumu kuita uchaguzi huo mwezi wa Juni kwa sababu ya kucheleweshwa harakati za kuwaandikisha wapiga kura na hali ngumu ya usalama, waliendelea kuarifu maafisa hao wa UM mjini New York. Kabla ya hapo Baraza la Usalama la UM lilirefusha kibali chake kwa harakati za wanajeshi wa UM nchini Afghanistan kwa mwaka mmoja mwengine, yaani hadi mwishoni mwa Machi 2005.