Ulaya yaunga mkono mkutano wa pande tatu kuhusu Ukraine
16 Agosti 2025Matangazo
Taarifa iliyotiwa saini na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer na rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, ilisisitiza kudumisha shinikizo kwa Urusi hadi amani ipatikane.
Trump na Putin Wakutana Bila Ukraine, Dunia Yatazama
Taarifa hiyo pia imeendelea kusema kuwa wataendelea kuimarisha vikwazo na hatua pana za kiuchumi ili kuweka shinikizo kwa uchumi wa kivita wa Urusi hadi amani ya kudumu itakapopatikana.
Viongozi hao wa Ulaya pia walisisitiza kuwa Urusi haiwezi kuwa na kura ya turufu juu ya Ukraine kujiunga na Umoja wa Ulaya au jumuiya ya kujihami ya NATO.