Ulaya: Hatua kali zichukuliwe na Marekani dhidi ya Urusi
20 Mei 2025Matangazo
Akizungumza Jumanne katika mkutano wa mawaziri wa umoja huo mjini Brussels, Kallas amesema Marekani ilisema kama Urusi haitokubaliana juu ya usitishaji mapigano bila masharti, basi hatua itachukuliwa.
Amesema hivyo wanataka kuona hatua hizo zikichukuliwa, pia kutoka upande wa Marekani.
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius amesema mazungumzo ya simu kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na Rais wa Urusi, Vladimir Putin yameonyesha kuwa Putin hayuko tayari kwa makubaliano ya dhati ya amani.
Aidha, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Mark Rutte amesema ni jambo zuri kwamba serikali ya Marekani inahusika katika juhudi za amani za Ukraine, lakini ni muhimu kwa Ulaya na Ukraine kuhusishwa pia.