Ulaya na Marekani wazungumzia mkataba wa biashara
5 Agosti 2025Matangazo
Sefcovic amesema anawasiliana na Howard Lutnick na Jamieson Greer, na kwamba mazungumzo hayo yanaendelea kwa ari ya kujenga.
Wakati huo guo, afisa wa Umoja wa Ulaya amesema ushuru wa asilimia 15 ambao bidhaa za umoja huo zitatozwa zinapoingia Marekani, unajumuisha wote, tofauti na makubaliano ambayo nchi nyingine zimefikia na Marekani.
Amesema mfumo wa ushuru utatumika kwa upana katika mauzo ya nje ya Umoja wa Ulaya, isipokuwa kwa chuma na aluminium.
Kiwango cha asilimia 15 pia kitatumika katika magari na vipuri vya magari, bila kuwepo viwango au kikomo.