Ukraine yatuma zaidi ya droni 100 kuelekea Urusi
28 Mei 2025Matangazo
Kwa mujibu wa maafisa wa Urusi, mashambulizi hayo ni sawa na yale yaliyofanyika wiki iliyopita, ambapo pia Moscow na miji mingine ililengwa.
Meya wa mji wa Moscow, Sergei Sobyanin, amesema kupitia mtandao wa Telegram kwamba vikosi vya wizara ya ulinzi vilizidunguwa droni 27 zilizokuwa zikielekea mji mkuu huo wa Urusi.
Soma zaidi: Urusi yasema mashambulio yake Ukraine ni ya kujibu uchokozi
Mapema, wizara hiyo ya ulinzi ilisema vikosi vyake vilizidunguwa droni 112 baina ya saa tatu na saa sita usiku wa kuamkia leo.
Urusi pia ilituma mkururo wa droni kuelekea Ukraine wiki iliyopita, ambapo Rais Volodymyr Zelensky alisema ndani ya siku tatu tu, Moscow ilisharusha zaidi ya droni 900 kuelekea Kiev.