MigogoroUlaya
Ukraine yashambulia mkoa wa Urusi wa Volgograd
19 Agosti 2025Matangazo
Maeneo yaliyozuka moto ni kituo kimoja cha kusafisha mafuta na pamoja na paa la hospitali moja kwenye mkoa huo.
Gavana wa mkoa huo, Andrei Bocharov amearifu kuwa wazimamoto walifika haraka kwenye maeneo hayo kuudhibiti moto huo na hadi sasa ripoti hakuna ripoti za majeruhi au kifo cha mtu.
Ukraine imesema ilifanya mashambulizi hayo ya droni ndani ya ardhi ya Urusi kujibu hujuma nzito za kijeshi zinazoendelea kufanywa na Moscow.
Imesema mashambulizi yake yananuwia kuharibu miundombinu inayolisaidia jeshi la Urusi ikiwemo vituo vya uzalishaji na usambazaji nishati.
Makabiliano kati ya pande hizo yanaendelea licha ya juhudi za kidiplomasia zilizoshika kasi kujaribu kumaliza vita kati ya nchi hizo mbili jirani vilivyodumu kwa muda wa miaka mitatu.