Ukraine yasema miundombinu yake ya gesi imeshambuliwa
11 Februari 2025Matangazo
Hayo yameelezwa na waziri wa nishati wa nchi hiyo pamoja na shirika la taifa la nishati na mafuta, Naftogaz. Inaarifiwa kwamba mashambulizi ya makombora ya Urusi yameulenga mkoa wa Poltava, na maeneo tisa katika moja ya wilaya za mkoa huo yamekosa usambazaji wa nishati ya gesi. Hata hivyo hakuna vifo wala majeruhi walioripotiwa kutokana na hujuma hizo. Katika miezi ya karibuni Urusi imeelekeza mashambulizi yake ya makombora na droni dhidi ya miundombinu ya kuchakata na kusambaza gesi nchini Ukraine baada ya hapo kuvilenga vituo vya kufua na kusambaza nishati ya umeme.