Ukraine yaripoti mapigano makali Donbass
31 Machi 2025Matangazo
Kupitia taarifa yake kwenye ukurasa wa Facebook, jeshi hilo limesema kumekuwapo matukio 104 ya makabiliano, ambapo mengi ya mashambulizi ya Urusi yalifanyika kwa mizinga na makombora.
Sehemu kubwa ya mapigano hayo yameripotiwa kutokea kwenye mji wa Pokrovsk kwenye jimbo la Donbass.
Mapema jana, mamlaka kwenye eneo hilo zilisema watu wawili waliuawa na wengine 35 kujeruhiwa kutokana na mashambulizi ya ndege zisizo rubani za Urusi kwenye mji wa mashariki mwa Ukraine wa Kharkiv.