Ukraine yaonywa juu ya mivutano manunuzi ya silaha
29 Januari 2025Matangazo
Maafisa hao wamesema hali hiyo inaweza kudhoofisha imani yao kwa nchi hiyo na kuitaka kutafuta suluhu haraka ili usivuruge usambazaji wa silaha.
Mvutano huo ulianza wiki iliyopita wakati bodi inayosimamia ofisi hiyo ya manunuzi ya silaha, kwa kauli moja kupiga kura ya kumrefushia mkataba, mkurugenzi wake Maryna Bezrukova.
Hata hivyo, Waziri wa Ulinzi Rustem Umerov alitupilia mbali uamuzi huo, akimshutumu kwa utendaji duni na kushindwa kufikisha silaha na risasi kwa wanajeshi waliopo mstari wa mbele, uamuzi ulioibua ukosoaji kutoka kwa wabunge na taasisi za kupinga rushwa waliosema hatua hiyo ni kinyume cha kisheria
Mzozo huo aidha unatokea wakati serikali mpya ya Rais Donald Trump ikihoji kuhusu msaada wa Marekani kwa Ukraine.