MigogoroUkraine
Ukraine: Urusi imemuua spika wa zamani wa Ukraine
1 Septemba 2025Matangazo
Andriy Parubiy, spika wa zamani wa bunge na kiongozi mkuu wa vuguvugu la maandamano ya Ukraine ya mwaka 2004 na 2014, aliuawa kwa kupigwa risasi katika mji wa magharibi wa Lviv unaopakana na Poland.
Polisi waliotangaza kumkamata mtuhumiwa huyo mapema leo, wamesema alimpiga risasi Parubiy mara nane jana mchana kabla ya kukimbia.
Taarifa ya Mkuu wa Polisi wa Kitaifa Ivan Vygivsky kwenye mitandao ya kijamii imesema wana uhakika kwamba shambulizi hilo halikuwa la bahati mbaya, na Urusi inahusika.
Mapema, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ukraine ilisema lilikuwa ni shambulizi la kupangwa, matamshi yaliyoungwa mkono na Rais Volodymyr Zelensky.