SiasaUkraine
Ukraine yahimiza vikwazo vya haraka dhidi ya Urusi
10 Julai 2025Matangazo
Zelensky amesema lazima shinikizo dhidi ya Urusi liwe na nguvu za kutosha ili nchi hiyo ione madhara ya ugaidi wake.
Urusi imeushambulia mji mkuu wa Ukraine, Kiyv kwa makombora 18 na droni zipatazo 400. Hayo ni mashambulizi ya pili makubwa ya Urusi dhidi ya Ukraine kuwahi kushuhudiwa mnamo siku za karibuni.
Rais wa Marekani, Donald Trump, ameidhinisha kupelekwa silaha za kujihami nchini Ukraine na anatafakari kuiwekea Urusi vikwazo vya ziada. Trump amesema amefadhaishwa na Rais wa Urusi, Vladimir Putin kuhusu kuongezeka kwa vifo katika vita vyake dhidi ya Ukraine.
Wakati huo huo, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, na wa Urusi, Sergei Lavrov, watakutana nchini Malaysia.