Ukraine yadai kuwarudisha watoto 12 waliochukuliwa na Urusi
4 Februari 2025Matangazo
Andriy Yermak, Mkuu wa Utumishi katika Ofisi ya Rais Volodymyr Zelensky, ameandika kupitia mtandao wa ujumbe wa Telegram kwamba hatua hiyo ni sehemu ya mkakati maalumu wa rais wa Ukraine wa kuwarejesha watoto waliokuwa chini ya udhibiti wa Urusi.
Vita kati ya Ukraine na Urusi bado kizungumkuti
Miongoni mwa watoto waliorejeshwa ni msichana mwenye umri wa miaka 16 aliyempoteza mama yake, binti wa miaka 17 aliyeitwa kujiunga na jeshi la Urusi na mtoto wa miaka minane.
Hata hivyo, ofisi ya mawasiliano ya Tume ya Haki za Watoto nchini Urusi imesema haina taarifa yoyote kuhusu watoto hao 12.